Habari ya leo rafiki yangu na mfatiliaji wa makala hizi bora kabisa za ujenzi. Ni matumaini yangu unaendelea kuchukua hatua muhimu ili kuhakikisha maisha yako na ya wale wanaokuzunguka yanakuwa bora kabisa!
Leo rafiki yangu karibu tujifunze kuhusu umuhimu wa kuweka
uzio kwenye eneo la ujenzi. Inawezekana umewahi kupita sehemu yenye ujenzi
ukakuta wamezungushia mabati kuzunguka eneo lote la ujenzi na ukawa unajiuliza
kwanini wamefanya hivyo? Kuna sababu nzuri tu kwanini eneo la ujenzi huwa
linazungushiwa uzio na hapa nakwenda kukueleza kwa kina sababu hizo. Lakini
kabla hatujajifunza sababu za uzio huu hebu tuone kwanza, **Uzio wa eneo la
Ujenzi (Site Hoarding), unamaanisha nini?**
Maana ya Uzio wa eneo la Ujenzi (Site Hoarding)
Huu ni aina ya uzio unaojengwa kwa matumizi ya muda mfupi
(temporary structure) kuzunguka eneo la ujenzi. Ujenzi wa uzio huu ni muhimu
sana na ni moja ya matakwa muhimu kutoka kwenye sheria za majenzi zinazotumika
sehemu mbalimbali. Uzio huu unaweza kujengwa kwa mabati (Hii ndo mara nyingi
inatumika), unaweza kujengwa pia kwa matofali au mabanzi kutegemeana na
ukubwa/umuhimu wa project. Uzio huu pia hujengwa kabla ujenzi haujaanza na
huondolewa pale ujenzi unapokamilika!
Kwanini kuweka uzio eneo la ujenzi??
Zifuatazo ni sababu muhimu za kuweka uzio kwenye eneo la
ujenzi;
1.
Sababu ya kwanza na kubwa ni USALAMA (Health
& Safety); uzio unahakikisha usalama wa wafanyakazi, wageni wanaokuja site
pamoja na wanajamii wanaozunguka eneo la ujenzi. Eneo la ujenzi linaweza kuwa
na mashimo, misumari, mizigo mizito… n,k hivyo usipoweka uzio ni rahisi kutokea
ajali za hapa na pale na ajali nyingine zinaweza kuwa mbaya kabisa.
2. Ulinzi na usalama wa mali zilizopo eneo la
ujenzi. Kwenye eneo la ujenzi huwa kuna malighafi mbalimbali za kujengea na
kama tunavyojua baadhi ya watu huwa sio waaminifu hivyo unapoweka uzio
unapunguza uwezekano wa kuibiwa malighafi za ujenzi!
3.
Kuhakikisha watu sahihi tu ndio wanaingia eneo
la ujenzi. Unapoweka uzio kunakuwa na geti maalumu la kuingilia na kutokea
hivyo ni rahisi kuhakikisha wale wanaohusika na ujenzi tu ndio wanakuwa kwenye
eneo la ujenzi.
4.
Kutumia sehemu hii ya uzio kuweka matangazo
yanayohusiana na kampuni inayofanya ujenzi wa mradi husika. Kampuni inayofanya ujenzi
inaweza kutumia uzio huu kujitangaza na kutafuta wateja zaidi kwa kuonyesha
kile wanachofanya na uwezo wao kwa ujumla. Hii ni njia rahisi kabisa ya
kujitangaza na kukuza biashara.
Rafiki hayo ndio mambo muhimu zaidi linapokuja swala la uzio
kwenye eneo la ujenzi. Zipo faida nyingine lakini kwa leo tuishie hapo. Cha
msingi unapojenga uzio hakikisha uzio huo uko imara ili usiezuliwe na upepo kirahisi au
kuharibiwa na watu kwa haraka. Uzio ni muhimu sana na unasaidia kutunza eneo lako
la ujenzi.
Kwa ushauri kuhusu maswala yote yanayohusiana na ujenzi
usisite kuwasiliana nami;
Rafiki yako mpendwa
Eng Beatus B. Laswai
Mobile
: 0752 655 084
Email
: engbeatus.laswai@gmail.com
0 comments:
Post a Comment